• complaint |
    • Wasiliana nasi |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
ASSOCIATION OF LOCAL AUTHORITIES OF TANZANIA-ALAT
ASSOCIATION OF LOCAL AUTHORITIES OF TANZANIA-ALAT

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania

  • Home
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Mission and Vision
  • Tunafanya nini?
    • Service one
    • Services two
  • Utawala
    • Organization Structure
  • Machapisho
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Utawala
    • Application Forms
  • Kituo cha Habari
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • Habari Mpya
    • Matukio
  • Projects
    • lic projects
  • Halmashauri

Historia

JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA 

(ALAT).

1:

ALAT ni nini?

ALAT ni kifupi cha "Association of Local Authorities of Tanzania" ambacho kwa kiswahili ni Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania. Jumuiya hii ilianzishwa tarehe 13 Desemba, 1984 mara baada ya kurejeshwa kwa Mfumo wa Serikali za Mitaa kwa Sheria Na. 7 na 8 za mwaka 1982.

Kwa hiyo, ALAT ni Jumuiya ya Halmashauri zote za Wilaya na za Miji, Miji Midogo na Vijiji Tanzania Bara.  Halmashauri za Miji ni pamoja na Majiji, Manispaa na Halmashauri za Miji.  Aidha, Halmashauri za Wilaya hujumuisha pia Serikali za Vijiji.

2:

Majukumu ya Jumuiya

 

Majukumu ya msingi ya Jumuiya hii kwa mujibu wa Katiba yake ni: usimamizi, uwakilishi, utetezi, ushawishi na utoaji huduma:

 

Usimamizi

 

ALAT ina jukumu la kusimamia kuwa wanachama wake wanatekeleza wajibu kwa mujibu wa sheria zao.

 
Uwakilishi:

Kwa jukumu hili Jumuiya hii huziwakilisha Serikali za Mitaa katika mikutano ya kitaifa na kimataifa inayohusu Serikali za Mitaa.  Aidha, ni jukumu lake pia kuwasilisha Serikalini maoni na mapendekezo ya Serikali za Mitaa kuhusu jambo lolote ambalo linaonekana ni la manufaa kwa wananchi.  


Utetezi 
Kwa jukumu  la utetezi ALAT hutetea haki na maslahi ya Serikali za Mitaa na huchukua kila hatua za lazima kuhakikisha kuwa haki na maslahi hayo yanalindwa.


Ushawishi

Kwa ushawishi ALAT inawashawishi watunge sera ama Watunga Sheria (Wabunge) kupitisha sera ama sheria kwa kuwa zina manufaa kwa Serikali za Mitaa au ina washawishi wahusika wasizipitishe kwa kuwa zinaathiri Serikali za Mitaa.


Utoaji huduma

Jukumu la ALAT la kutoa huduma kwa Halmashauri ni pamoja na kutafuta na kupata habari, ushauri na maoni ya kitaalam kuhusu serikali za mitaa na kuyasambaza kwa wanachama. Huduma nyingine ni pamoja na utoaji wa mafunzo ya ujengaji uwezo kwa Madiwani na Watendaji wao, ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.


Usambazaji wa habari

Jukumu lingine la ALAT ni kusambaza habari zozote muhimu zihusuzo Serikali za Mitaa kwa Halmashauri wanachama na umma kwa jumla kwa njia ya nyaraka, radio na makala na kwa Jarida la ALAT n.k. Kwa njia hii. Halmashauri zinaweza pia kupashana habari na kubadilishana uzoefu juu ya shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Halmashauri zao hususan kuhusu mifano bora ambayo inafaa kuigwa.

Matangazo

  • MAPATO YA NDANI YA HALMASHAURI. March 17, 2022
  • View All

Latest News

  • MAADHIMISHO YA MWAKA MMOJA WA KIFO CHA ALIYEKUWA RAIS WA AWAMU YA TANO.

    March 17, 2022
  • MAPATO YA NDANI YA HALMASHAURI.

    March 17, 2022
  • PONGEZI KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO.

    February 20, 2022
  • Viongozi wa ALAT TAIFA wawashukuru Benki ya NMB.

    February 17, 2022
  • View All

Video

mikumi
More Videos

Quick Links

  • ALAT

Related Links

  • TAMISEMI
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Jengo la Sokoine,Barabara ya CDA Dodoma

    Postal Address: P.O.Box 2049 DODOMA

    Telephone: 0262323407

    Mobile: +255(0)754283505

    Email: alat_tz@yahoo.com au moses.kaaya@gmail.com

Mawasiliano mengine

   

Wanaotembelea

Visitors Counter

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2018 ALAT . All rights reserved.