Jumuiya ya Tawala za MitaaTanzana (ALAT) imeishukuru Benki ya NMB kwa kukabidhi hundi yenyethamani ya Sh. Mil. 120 ili kudhamini Mkutano Mkuu wa 38 wa Mwaka waJumuiya hiyo unaofunguliwa leo katika Hoteli ya Golden Tulip iliyopo mjini Zanzibar,
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo, Makamu Mwenyekiti wa ALAT Mhe.Sima Constantine Sima ameishukuru Benki ya NMB kwa kuendelea kufanikisha vikao na Mikutano Mikuu ya kila mwaka ya ALAT kwa kipindi cha miaka nane sasa ya udhamini wao.
Amesema inachofanya Benki ya NMB katika kufanikisha Mikutano Mikuu ya ALATTaifa kwa miaka nane sasa ndio tafsiri sahihi ya mahusiano mema naya muda mrefu ambayo ALAT wamekuwa wanufaika wakuu.
“NMB sio tu wadau wetu kibiashara, bali wamekuwa moja ya sehemu kuu za sisi kutolea huduma zetu. Mambo mengi yanayoendelea kufanyika katika Halmashauri zetu yanapitia kwao na ndio ushuhuda wa hili na mahusiano haya ndio tafsiri sahihi ya tunayoyaona kwa miaka nane ya udhamini wao,” ameeleza Mhe.Sima na kuongeza:
“Nichukue nafasi hii kuishukuru NMB kwa kutafsiri kwa vitendo juu ya mahusiano mema, ambapo leo pia imedhamini uzinduzi wa kimapinduzi wa Mamlaka zaSerikali za Mitaa Zanzibar (ZALGA), ambayo ni mamlaka sawa na ALAT kwa huku visiwani Zanzibar.”
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna ambaye ndiye aliyekabidhi hundi hiyo ameeleza kuwa Benki ya NMB inajivunia kuwa mbia mkubwa wa ALAT, na kwamba Benki hiyo inathamini heshima ya kipekee inayopewa na uongozi wa jumuiya hiyo.
“NMB tunajivunia ubia baina ya benki yetu na Jumuiya hii, lakini pia tunathamini sana heshima ya kipekee ambayo tumekuwa tukipewa na Uongozi wa ALAT Taifa ya kujumuika pamoja nao katika Mkutano Mkuu huu muhimu kwa maendeleo ya Halmashauri zetu nchini.
“Kwa siku zote za Mkutano Mkuu wa ALAT, tutakuwa na banda letu nje ya ukumbi wa mkutano, ili kuhakikisha wajumbe wa kikao pamoja na wadau wengine watakaokuwa katika maeneo ya Golden Tulip Hotel, wanapata huduma za kifedha wakati wote wa kikao,” amesema Bi Zaipuna.
Mkutano Mkuu wa 38 wa Mwaka wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), unafunguliwa Leo Jumanne Aprili 23 na Rais Dkt. Samia SuluhuHassan, ambapo unawakutanisha zaidi ya washiriki 600.
Mkutano Mkuu wa ALAT, unawapa fursa viongozi wa Serikali Kuu kutoa Maelekezo na Miongozo ya Kisera kwa Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa,wakiwemo Mameya wa Majiji na Manispaa, Wenyeviti na Wakurugenzi waHalmshauri 184 (za Tanzania Bara), na utafungwa Aprili 25 na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Hafla hiyo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa ALAT Mhe.Sima Constantine Sima pia ilihudhuriwa na Kaimu Katibu Mkuu wa ALAT Taifa Bw. Mohamed Maje na baadhi ya Wajumbe wa Kamati tendaji ya jumuiya hiyo
Jengo la Sokoine,Barabara ya CDA Dodoma
Postal Address: P.O.Box 2049 DODOMA
Telephone: 0262323407
Mobile: +255(0)784209840 au
Email: alat_tz@yahoo.com
Copyright ©2018 ALAT . All rights reserved.